DIGITAL ONLINE SALES

HUDUMA ZETU & VIGEZO

HUDUMA ZA VODACOM

DIGITAL ONLINE SALES, Tupo kwaajiri yako na tutahakikisha unapata huduma bora za LIPA kwa M-PESA kutoka Vodacom. Tunawezesha tunawawezesha wafanya biashara wa aina zote, kuanzia wadogo, wakati na wafanya biashara wakubwa. hivi hapa vigezo vya kupata lipa kwa M-PESA.

Kigezo cha kwanza uwe na tin namba. Kama hauna TIN NAMBA, usijari utatengenezewa

Kigezo cha pili uwe na namba ya nida au kitambulisho cha nida.

baada ya apo, SAJIRI LAINI MPYA ya voda, zingatia ukisha sajiri laini hiyo ya voda usiiwezeshe upande wa m-pesa yaani USIIWEKEE NAMBA YA SIRI AU PIN. namba ya siri utaweka baada ya lipa namba yako kukamilika
kwahio sasa unachotakiwa kufanya mara baada ya kuisajiri laini yako weka vocha ya kukwangua ya elf 1000 au ya mia 500.

Baada ya hapo ntumie majina ako yote matatu kwa usahihi bila kuyakosea. pia ntumie picha yako ya mfumo wa passport size, jipige picha kwa kutumia simu yako.

VIGEZO NI HIVYO BOSS... Karibu sana!!

Wasiliana nasi WhatsApp

HUDUMA ZA AIRTEL

Maelekezo ya Kupata Laini ya Uwakala wa Airtel Money na Lipa Namba

Vigezo vya Kupata Laini ya Uwakala wa Airtel Money

Vigezo vya Kupata Lipa Namba ya Airtel

⚠ Zingatia Masharti Haya ⚠

  • Kama laini yako ni mpya, hakikisha:
    • Umeweka vocha na kuunga kifurushi chochote cha kuanzia Tsh 500 na kuendelea.
    • Akaunti ya Airtel Money imefunguliwa au imewezeshwa (uweke namba ya siri ya Airtel Money).
  • Laini yako haipaswi kuwa na:
    • Huduma ya SME.
    • TILL ya uwakala wa Airtel Money.
    • Lipa Namba nyingine iliyosajiliwa kwa majina yako au NIDA yako.

HUDUMA ZA HALOTEL

Je, unahitaji laini yako iwe ya uwakala wa Halopesa? Tunakupa fursa ya kuboresha biashara yako kwa kukusaidia kupata huduma hii kwa urahisi. Hakikisha unakidhi vigezo vilivyowekwa ili kufanikisha mchakato wa usajili.

Vigezo vya Kupata Laini ya Uwakala wa Halopesa

  • Uwe na TIN Namba: Hii ni muhimu kwa usajili wa kibiashara.
  • Kitambulisho.: Hakikisha una kitambulisho cha mpiga kura au kitambulisho cha NIDA.
  • Mtaji wa Awali: Kwenye akaunti yako ya Halotel, hakikisha kuna kiasi cha shilingi laki moja (Tsh 100,000).
    • Kiasi hiki ni mtaji wako wa awali wa float kwa ajili ya kukamilishia Till yako Halopesa.
    • usajili ukisha kamilika baada yako utaruhusiwa kuitoa float yako.

Zingatia

Bila kuwa na shilingi laki moja kwenye akaunti yako ya Halotel, laini ya uwakala haiwezi kutengenezwa. Maombi yatakayokosa vigezo hivi yatakataliwa mara moja (Rejected❌).

Je, Unahitaji Msaada Zaidi?

Kwa maelezo zaidi au msaada wa haraka, wasiliana nasi kupitia njia zetu za mawasiliano. Tunatoa huduma za kitaalam kuhakikisha mchakato wako unakamilika kwa mafanikio.

Jiunge nasi leo na uanze safari yako ya mafanikio na Halopesa!

Wasiliana nasi WhatsApp

HUDUMA ZA ZIADA.

Tunajitahidi kutoa huduma bora za kusaidia wateja wetu kufanikisha malengo yao ya biashara na kuepuka changamoto katika masuala mbalimbali ya uwakala, usajili wa biashara, na uboreshaji wa masoko. Huduma zetu ni zenye ubunifu na gharama nafuu.

Huduma Tunazotoa

  • Kukabiliana na Changamoto za Uwakala na Lipa Namba
    Tunakusaidia kutatua matatizo yote yanayohusiana na huduma za uwakala na Lipa Namba. Ikiwa unahitaji msaada wa kiufundi au maelezo kuhusu namna ya kusimamia huduma hizi, sisi ndio suluhisho lako.
  • Utengenezaji wa TIN Namba
    TIN Namba ni muhimu kwa shughuli za kibiashara na kodi. Tunakusaidia kupata TIN Namba kwa urahisi, pamoja na kutoa elimu kuhusu umuhimu wake na jinsi inavyoweza kukuza biashara yako.
  • Kupata Leseni ya Biashara
    Tunatoa mwongozo kamili wa hatua za kupata leseni ya biashara. Huduma hii inalenga kuhakikisha biashara yako inasajiliwa kihalali na ina uwezo wa kufanya kazi bila changamoto za kisheria.
  • Usajili wa Jina la Biashara (BRELA Registration)
    Tunaelewa kuwa kusajili jina la biashara yako ni hatua muhimu katika kuanzisha biashara rasmi. Tunakusaidia mchakato mzima wa usajili kupitia BRELA kwa urahisi na haraka. kwa gharama ya TSH 25,000/= TU
  • Huduma za Graphic Design na Website Design
    Tunatengeneza miundo bora ya picha na tovuti ili kuhakikisha biashara yako inaonekana kitaalam mtandaoni. Tunazingatia mahitaji yako na tunatoa huduma kwa bei nafuu na ubora wa hali ya juu.
  • Elimu Kuhusu Biashara za Mtandaoni
    Biashara za mtandaoni zimekuwa na umuhimu mkubwa katika uchumi wa kisasa. Tunatoa mafunzo maalum ya jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara zako mtandaoni kwa mafanikio makubwa.
  • Matangazo ya Biashara Kupitia WhatsApp Bulk Sender
    Tunakusaidia kutumia mfumo wa WhatsApp Bulk Sender ili kutangaza bidhaa na huduma zako kwa wateja wengi mara moja. Mfumo huu unasaidia kufikia wateja wengi kwa gharama nafuu na kwa urahisi.
  • Mafunzo ya WhatsApp Automatic Reply System
    Tunatoa mafunzo ya jinsi ya kutumia na kusanidi mfumo wa WhatsApp Automatic Reply. Mfumo huu unakusaidia kujibu wateja wako kwa haraka na kitaalam hata kama haupo mtandaoni. Gharama ya mafunzo ni Tsh 85,000/=.

    Mfumo huu ni muhimu kwa biashara zinazopokea maombi au maswali mengi kutoka kwa wateja.

ELIMU KUHUSU BIASHARA YA UWAKALA

Ukiwa Kama wakala wa mtandao wa Airtel,M-PESA, na HALOTE,au hata kwa mitandao mingine unapaswa kufahamu wajibu wako kama mtoa huduma.
hivyo basi kazi yako ni kuhakikisha, huduma zinawafikia wateja kwa haraka, usalama na ufanisi. sisi kama DIGITAL ONLINE SALES tutakupa elimu kwa ufupi kuhusu biashara hii ya uwakala.

MHIMU KUZINGATIA.

  1. kitu cha kwanza, elewa mfumo mzima wa utoaji huduma kwa kila Mtandao.
    • Airtel money: unapaswa kufahamu matumizi sahihi ya flot, jinsi ya kuhudumia mteja anae taka kutoa pesa pia mteja wa kutuma pesa, kulipia huduma mbalimbali mfano, luku, bill na malipo mengine ya serikali.
    • Halopesa: Huduma zinazo jumuisha kutuma pesa, kutoa pesa, kulipia bili na kununua vocha za simu.
    • M-pesa: kuhusu miamala ya pesa, matumizi sahihi ya huduma ya voda rusha kwa kutumia menyu ya *150*00*50# pia matumizi ya wakala songesha.

      Kwa elimu na msaada zaidi wasiliana kupitia whatsapp namba 0785106106.
      Anzisha mazungumzo kwa kuandika hello kisha utajibiwa AUTOMATIC, baada ya hapo fuata maelekezo ya mfumo. andika YES au NO kisha fuata maelekezo ili uweze kujihudumia kwa haraka na kwa ufanisi wa haki ya juu. ahsante kwa kuchagua huduma zetu kutoka DIGITAL ONLINE SALES.

      © 2025 All rights reserved

      Chat with us on WhatsApp
      Chat with us